bobi

Bobi Anayeongea

Dogo mmoja alifanikiwa kuingia chuo kimojawapo nchini kwa mbwembwe sana. Katikati ya simesta, dogo akaishiwa hela na akaamua kumwandikia baba yake barua.

“Kwako baba,

Ni matumaini yangu hujambo. Huku chuoni mambo ni mazuri sana. Kuna maajabu hapa maprofesa hapa wamegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea.  Mlete Bobi na shilingi laki 5, baada ya muda atakuwa anaweza kuongea.

Ni mwana’ko Dogo.”

Mzee wa watu haraka akatuma mkwanja na mbwa wake chuoni. Haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Dogo akamtumia baba yake barua nyingine kuwa walimu wameboresha programu kwani sasa wanaweza kumfundisha mbwa kusoma.

Mzee wa watu akaongeze kimilioni bila hiyana. Mzee huyu aliyekuwa tayari anajisifu kijiji kizima akauza ng’ombe akatuma mkwanja.

Likizo ikafika Dogo akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake. Alipofika tu baba yake akamuulizia Bobi wake. Denti akamuita baba yake pembeni.

Dogo: Baba hili nitakalokwambia sitaki mama asikie?.

Baba:Vipi tena??

Dogo: Jumapili iliyopita tumeamka vizuri na Bobi, yeye kama kawaida yake akaenda kuchukua gazeti la Mzalendo na kukaa kwenye kiti na kuanza kusoma, ghafla wakati anasoma akaniita akanambia hivi, “baba yako bado anaendelea na kale kachangudoa ka pale mtaa wa pili?”Nilishtuka!

Baba: (Akaingilia kati) Ungemwua hapo hapo mbwa mshenzi huyu anataka kuniharibia mambo yangu!

Dogo: Baba na mimi lilinijia wazo ilo hilo sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa!

Baba: Safi sana safi sana, wewe jembe langu!

Comments

comments