sikio

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya bosi wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili bosi asigundue. Mara kadhaa bosi alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu na alihisi Bakari tu ndiye anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndio mchakachuaji, bosi alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.


Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Bosi: Bakariiii!

Bakari: Naam baba!

Bosi: Nani anakunywa wine yangu?

Bakari: (Kimyaaaa hajibu kitu!)

Bosi: Bakariiiii !

Bakari: Naam baba!

Bosi: Nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!

Bakari: (Kimyaaaaa!)

Bosi akaamua amfuate hukohuko jikoni.

Bosi: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?

Bakari: Baba huku jikoni ndivyo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno mengine husikii, na kama huamini baki jikoni mimi niende sebuleni. (Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita!)


Bakari: Babaa!

Bosi: Naam Bakari!

Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Bosi: (Kimyaaaa!)

Bakari: Baba babaa!

Bosi: Ndio Bakari!

Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?

Bosi:  (Kimyaaaaaaa! Boss akatoka nje)  Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.

Mama akasema msinizingue nyie…!! Mbona siwaelewi!


Bakari: Mama kama uamini na wewe nenda uone.

Mama akaenda jikoni..

Bakari: (Akaita) Mamaa

Mama: beeee Bakari

Bakari: Eti hiyo mimba ni ya baba au yangu.?

Mama:  (Kimyaaaa)

Bakari:  Mama nauliza tena hiyo mimba ni ya baba au yangu?

Mama:  (Akatoka) Aisee kweli humu unasikia jina tu!

**********

Comments

comments