babu na viatu

Kuna babu mmoja alikutwa stendi ya mabasi analia sana. Wasamaria wema wakaamua kumsaidia yule babu lakini kila walipokuwa wakimwuliza,

“Babu unalilia nini?”

akawa hasemi anaendelea kulia tu, wasamaria wema wakaamua kumbeba hadi hospitali. Walipofika hospitali daktari akamwuliza babu tatizo lake ili aweze kumsaidia,


Daktari: Mzee unaumwa nini?

Babu: (Akaendelea kulia kwa muda)

Daktari: Eti babu yangu nini kinakusumbua? Unaumwa nini nikutibu?

Babu: SIUMWI ILA VIATU VINANIBANA SANA!!!!

**********


Comments

comments