Anko Magu Kutumbua Majibu

Afrika Mashariki

Magu

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeendelea kuipa Tanzania nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo. Katika mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kilichokutana jana huko Arusha Tanzania kilimchagua Rais wa Tanzania kuendeleza uenyekiti ambao ulikuwa chini ya Jakaya Mrisho Kikwete, Rais mstaafu wa Tanzania.

Rais Magufuli amejipatia umaarufu mkubwa Afrika na dunia nzima kwa kuonesha nia yake ya dhati kabisa katika kubadili maisha ya Watanzani. Akihutubia wakazi wa Arusha, Magufuli alisema hajui kwa nini kachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ila kwake yeye ni kazi tu. Akaonya kuwa akiyaona majipu katika nchi za jumuiya wanachama wampe ushirikiano kwa kuyatumbua majipu yao.

Pia Sudan ya Kusini ilipewa uanachama wa Afrika Mashariki na kufanya jumuiya hiyo kufikisha nchi saba mpaka sasa.  Hii hapa video yake!

Comments

comments