Akili Za Mataputapu Ni Shida

mlevi

Nyumbani kwa mlevi mmoja, kuna shimo kubwa nje ya nyumba yake ambalo huwa linajaa maji yasiyokauka kwa muda mrefu. Siku moja mlevi huyo alirudi usiku wa manane akiwa chakari kwa mataputapu. Na mambo yalikuwa kama hivi;

Mume: Fungua mlango!

Mke: Leo sifungui, nimechoshwa na ulevi wako.

Mume: Kama ufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisaaaaa!

Mke: Kufa huna faida yoyote duniani.

Basi mume akachukua jiwe kubwa sna na kulitupia katika shimo, dumbwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Mke akajifunga kanga moja haraka haraka na kufungua mlango. Ghafla mume akaingia na kumfungia mkewe nje!

Mke: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje!

Mume: Piga kelele na wakija waambie unatoka wapi usiku huu na kanga moja!

Mke: Basi naenda kulala kwa Tito ( Jirani ambaye hajaoa)

Mume: Weeeeeeeeeeeeeeeeee! Subiri nife ndo ukalale kwake, hebu ingia ndani! (Huku anafungua mlango.)

Nani mkali?

Comments

comments