Jamaa alipoteza mali zote na akawa masikini wa kutupwa kwa sababu ya ulevi. Jambo hili lilimsononesha sana kiasi akawa anachukia sana pombe.

Siku moja akapita karibu na jalala akaona chupa za Bia. Ikabidi alisogelee jalala ili azione vema zile chupa. Akaishika ya kwanza akaipasua, huku akisema, “kwa sababu yako nimeachana na Mke wangu.”

Akashika ya pili na kuipasua huku akasema, “kwa sababu yako nimeshindwa kusomesha wanangu!”


Akashika ya tatu akiwa na hasira akasema, “kwa sababu yako nimefukuzwa kazi”, akaipasua!

Ya nne akasema, “kwa sababu yako nimeuza gari, nyumba, shamba na nali zote mpaka nimefilisika”, akaipasua.

Akashika ya tano na akakuta imejaa bia akasema, “wewe kaa pembeni kwanza huu ugomvi haukuhusu, tutaongea baadae.”

HIHIHIHIHIHIHI CHEZEA BIA WEWE?!

**********


Comments

comments