Livingstone

Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la James nusura atokwe roho kwa mshtuko kutokana na tabia yake ya kujisifi sanaaaaaaaa! James hakubahatika kusoma wakati wa udogo wake hivyo aliamua kujiendeleza wakati anafanya kazi. Ilikuwa ni kawaida yake kila siku milango ya saa kumi na moja jioni anaenda kusoma!


Mkasa huo uliokea siku moja ambapo ilikuwa ni kawaida ya James kujisifia kila mara:

James : Wiki ijayo nafanya mtihani, ni miezi sita sasa nafanya masomo ya jioni, nimejua mengi sana, we unamjua David Livingstone?

David : Hapana simjui!

James : Huyo ndiye mzungu wa kwanza kuliona Ziwa Victoria, ungekuwa unasoma masomo ya jioni ungemjua huyu.

Haya ni baadhi ya maswali ambayo alikuwa anayauliza kila siku kazini. James akawa kero kazini kwa maswali yake na yakawa yanamkera sana Davidi.

James : We unamjua Graham Bell?


David : Hapana simjui!

James : Huyo ndie alikuwa mtu wa kwanza kutengeneza simu, ungekuwa unaenda kuchukua masomo ya jioni ungemjua.

Siku moja David akamwita James;

David : Jemsi unamjua Hassan Makolokocho?

James : Hapana! ndiyo nani huyo?

David : Huyo ndiye mchepuko wa mkeo kwa miezi sita sasa, ungekuwa huendi kuchukua masomo ya jioni ungemjua!

**********


Comments

comments